Kesi
inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha upinzani CHADEMA Tundu Lissu,
imeahirishwa hadi Jumatatu ya Agosti 17 baada ya Shahidi wa 18 kati ya
30 aliyetakiwa kutoa ushahidi wake leo kupata dharura ya kiafya.
GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA CHUMBANI NA KAMA UNAHITAJI AJIRA SASA
Akitangaza
Mbele ya jopo la majaji watatu, wakili mwandamizi wa Serikali amesema
shahidi huyo amehudhuria Clinic katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kutokana na changamoto ya kiafya.
Wamesema hata mashahidi ni
binadamu, hivyo changamoto ya kiafya inaweza kumtokea yeyote huku
wakiahidi kuja na mashahidi wote waliobaki Jumatatu ya Agosti 17,2026.
Hata
hivyo mshitakiwa Tundu Lissu, amepinga vikali ombi hilo la upande wa
Jamhuri huku akisema kuwa, wanafanya hivyo kwa vile Mahakama haichukui
hatua yoyote kwani ilishatoa maelezo kwa upande wa Jamhuri kuja na
mashahidi kuanzia wawili.
Mshitakiwa Tundu Lissu, amesema kama
upande wa Jamhuri hauwezi kuendelea 'akitumia neno "Pumzi kukata", basi
wafunge mashahidi na kuendelea hatua nyingine.
Hata hivyo jopo la
majaji watatu likiongozwa na Dustan Ndunguru imekubaliana na ombi la
upande wa Jamhuri na kuagiza upande wa Jamhuri kuja na mashahidi wote
Jumatatu ya Agosti 17.
Lissu ambaye leo anatimiza siku 493 akiwa
gerezani, jana alimhoji shahidi wa 17 wa siri aliyepewa jina la P,
ambaye alianza kutoa Ushahidi wake kabla ya kufanyiwa maswali dodoso.
Lissu
anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)(d)
cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalotokana na maneno aliyoyatamka
kuhusiana na kusudio la kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka
2025.
0 Comments