Mkurugenzi wa Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF), Eng. Maryprisca Mahundi (ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu), anatarajiwa kuleta tabasamu na chachu mpya ya michezo kwa vijana wa Kata ya Iwambi, Jijini Mbeya.
Katika muendelezo wa kuinua vipaji na kuwezesha jamii, Eng. Mahundi kupitia taasisi yake ya MWEF ataongoza zoezi la kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu za Kata hiyo.
📍 TAARIFA ZA TUKIO:
Mgeni Rasmi: Eng. Maryprisca Mahundi (Mkurugenzi wa MWEF na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu)
Tarehe: Jumamosi, 15 Agosti, 2026
Muda: Kuanzia Saa 08:00 Mchana
Eneo: Uwanja wa Shule ya Sekondari Iwambi, Mtaa wa Lumbila
⚽ Lengo la Tukio
Hafla hii inalenga kusaidia maendeleo ya michezo kwa vijana, kukuza afya, na kujenga ushirikiano pamoja na nidhamu kupitia michezo katika Kata ya Iwambi na Jiji la Mbeya kwa ujumla.
"KAZI NA UTU – TUNASONGA MBELE!"
Wananchi na wapenda michezo wote mnakaribishwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Mgeni Rasmi na kuunga mkono michezo katika kata yetu.

0 Comments