TAHARUKI:MTOTO WA MIEZI 4 AACHWA KWA MAMA ASIYEMFAHAMU

 Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi minne ametelekezwa katika kituo kidogo cha magari ya abiria kinachosafirisha abiria kutoka Babati kuelekea Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.

GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA CHUMBANI NA KAMA UNAHITAJI AJIRA SASA. 

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, mtoto huyo alitelekezwa na abiria mmoja aliyedai kuwa anatokea Arusha na alikuwa akisafiri kuelekea Mwanza.

Abiria huyo alimkabidhi mtoto kwa mama mmoja mjasiriamali, Glory Lazaro, aliyekuwa akifanya biashara ya kuuza bidhaa mbalimbali katika kituo hicho, kisha akaendelea na safari bila kurejea kumchukua mtoto huyo.

Glory amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi jioni, Agosti 15, 2026, na tangu wakati huo amekuwa akimsaidia mtoto huyo licha ya kukabiliwa na changamoto za kifedha. Amesema tayari ana watoto watano anaowahudumia, hivyo kuongeza jukumu la kumlea mtoto huyo kumemuweka katika mazingira magumu.

Kutokana na hali hiyo, Glory ameiomba Serikali, mamlaka husika pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kumsaidia katika malezi na mahitaji muhimu ya mtoto huyo, huku akisisitiza kuwa hana uwezo wa kifedha wa kumlea peke yake. Pia ametoa wito kwa jamii kushirikiana kuhakikisha mtoto huyo anapata malezi salama, huduma muhimu na haki zake za msingi.

Post a Comment

0 Comments