TANZANIA YAKANUSHA TUHUMA ZA KUVURUGA UCHAGUZI WA ZAMBIA

Na Ally Mandai.

Serikali ya Tanzania imekanusha vikali tuhuma zinazodai kuwa imewatuma watu nchini Zambia kwa lengo la kuingilia au kuvuruga uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Agosti 13, 2026.

GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA CHUMBANI NA KAMA UNAHITAJI AJIRA SASA

Tuhuma hizo zilitolewa na mgombea urais wa chama cha NRPUP nchini Zambia, Bw. Brian Mundubile, ambaye alidai kuwa Tanzania imetuma watu nchini humo kwa ajili ya kuingilia mchakato wa uchaguzi.

Hata hivyo, Serikali ya Tanzania imesema tuhuma hizo hazina ukweli, huku ikizichukulia kwa uzito na kuchukua hatua za kutaka ufafanuzi rasmi kutoka kwa Serikali ya Zambia.

Kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, Serikali imewasiliana na Serikali ya Zambia ikiomba maelezo ya kina kuhusu tuhuma hizo pamoja na sababu zilizomfanya mgombea huyo kutoa madai hayo dhidi ya Tanzania.

Serikali imesisitiza kuwa Tanzania haijamtuma mtu yeyote kwenda Zambia kwa ajili ya kuingilia, kuvuruga au kuathiri uchaguzi huo, na kwamba hatua kama hiyo haiendani na utamaduni wala misingi ya Tanzania katika mahusiano yake na nchi jirani.

Aidha, Tanzania imeeleza kuwa kama ilivyo kwa nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ina uwakilishi wa waangalizi wa uchaguzi nchini Zambia.

Waangalizi hao, kwa mujibu wa Serikali, wanafanya kazi kwa kuzingatia miongozo na taratibu za waangalizi wa uchaguzi wa SADC, sambamba na waangalizi wengine wa kimataifa na wa ndani waliopo nchini Zambia.

Serikali imefafanua kuwa uwepo wa waangalizi hao hauhusiani na kuingilia uchaguzi, bali ni sehemu ya jukumu la uangalizi wa mchakato wa uchaguzi kwa mujibu wa taratibu za SADC.


Tanzania imewahakikishia Watanzania pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kuwa inaheshimu mamlaka, uhuru na taratibu za uchaguzi za Zambia, na haina nia wala mpango wa kuingilia mchakato wa kisiasa wa nchi hiyo.

Kauli hiyo imekuja wakati Zambia ikimaliza mchakato wa uchaguzi uliofanyika Agosti 13, 2026, huku macho ya ukanda wa SADC yakiwa kwenye mwenendo na matokeo ya uchaguzi huo

Post a Comment

0 Comments