Kupitia
ukurasa wake rasmi wa instagram, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt.Emmanuel Nchimbi, ametangaza uamuzi wake wa kustaafu
rasmi siasa na utumishi wa umma, akitarajia kujiuzulu nafasi hiyo
kuanzia tarehe 4 Septemba 2026 kwa mujibu wa Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa
pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya nchi.
Kupitia barua
aliyomwandikia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Agosti 25, 2026,
ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kutimiza ahadi aliyoiweka ya kuachia
ngazi wakati wowote mkuu huyo wa nchi atakapohitaji mabadiliko katika
nafasi hiyo.
Kiongozi huyo ametoa shukrani za dhati kwa Rais
Samia na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa imani kubwa waliyompa, huku
akiwashukuru Watanzania wote kwa ushirikiano waliomwonyesha katika
kipindi chote cha utumishi wake.
Aidha, amesisitiza kuwa ataendelea kuwa raia mwema na mtiifu kwa taifa lake mara baada ya kuhitimisha majukumu yake serikalini.
TAARIFA RASMI YA SERIKALI ITATOLEWA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA
0 Comments