ANAYETUHUMIWA KUCHOMA MAHAKAMA MBARONI MOSHI

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia John Daud (42), mkazi wa Mtaa wa Lenguwa wilayani Moshi, kwa tuhuma za kuchoma moto jengo la zamani la Mahakama ya Mwanzo ambalo halitumiki kwa sasa.

Tukio hilo lilitokea Agosti 24, 2026 asubuhi na kusababisha vyumba vinne pamoja na nyaraka zilizokuwemo ndani kuteketea, kabla ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi kufanikiwa kuuzima bila kuleta madhara kwa binadamu huku thamani ya mali zilizoharibika ikiwa bado haijafahamika.

Kufuatia tukio hilo, polisi walianzisha msako mkali na kufanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo Agosti 25, 2026 akiwa kwenye hafla ya Maulidi.

Jeshi hilo limeeleza kuwa uchunguzi wa kina unaendelea kwa ushirikiano na vyombo vingine vya kiusalama, na mara utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka yanayomkabili.

Post a Comment

0 Comments