Mtu mmoja
anayedaiwa kuwa na tatizo la ugonjwa wa akili amechoma moto kwa jengo la
zamani la Mahakama ya Mwanzo Moshi, mkoani Kilimanjaro, na kusababisha
vyumba vinane (8), nyaraka za Mahakama pamoja na sehemu ya jengo la
Ustawi wa Jamii kuteketea kwa moto.
.jpeg)
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremia Mkomangi, amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kusema askari wa zimamoto walifika katika eneo la
tukio na kufanikiwa kuuzima moto huo.
Kwa mujibu wa Mkomangi,
moto huo ulisababisha kuungua kwa ofisi moja ya jengo hilo pamoja na
chumba kilichokuwa kikihifadhi nyaraka za mahakama, na kusababisha
nyaraka zilizokuwamo kuteketea.
Amesema uchunguzi wa awali
unaonesha kuwa moto huo ulisababishwa kwa makusudi, huku mtu mmoja
anayesadikiwa kuwa na changamoto za afya ya akili akihusishwa na tukio
hilo.
“Vyumba vinane vya Mahakama ya Mwanzo pamoja na nyaraka
zake zote na jengo la Ustawi wa Jamii Moshi vimeungua. Chanzo cha moto
huo ni kuchomwa kwa makusudi na mtu anayesadikiwa kuwa na tatizo la
akili,” amesema Mkomangi.
0 Comments