Mahakama
nchini Syria imemhukumu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Bashar al-Assad,
adhabu ya kifo baada ya kupatikana na hatia ya makosa mbalimbali
yaliyohusishwa na ukandamizaji na vita vya wenyewe kwa wenyewe
vilivyotikisa nchi hiyo kwa takribani miaka 14.

Hukumu hiyo
ilitolewa Jumanne, Agosti 11, 2026, na inakuwa hukumu ya kwanza kubwa ya
ndani dhidi ya Assad tangu kuondolewa kwake madarakani mwaka 2024.
Assad
akuwapo mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo. Tangu serikali
yake kuangushwa mwezi Desemba 2024, amekuwa akiishi nchini Urusi baada
ya kukimbilia huko kufuatia kuanguka kwa utawala wake.
Mahakama
pia imemhukumu kifo Maher al-Assad, ambaye ni kaka yake Bashar, pamoja
na Atef Najib, aliyekuwa mkuu wa usalama wa kisiasa katika mkoa wa Daraa
na binamu wa Bashar al-Assad.
Tofauti na Bashar na Maher, Atef
Najib alikuwepo mahakamani wakati hukumu ikisomwa. Najib alihusishwa na
operesheni za ukandamizaji dhidi ya waandamanaji katika Daraa mwaka
2011, eneo ambalo lilikuwa miongoni mwa vituo vya mwanzo vya maandamano
yaliyokuja kuchochea vita vya Syria.
Kwa mujibu wa taarifa za
mahakama, mashtaka dhidi ya Assad yalihusisha mauaji, mateso, kukamatwa
kiholela na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa wakati wa vita vya
Syria
0 Comments