Yanga SC imeifunga Simba SC kwa bao 1-0 na kutwaa Ngao ya Jamii 2026 katika mchezo uliochezwa usiku huu kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA YAKO CHUMBANI SASA
Albert Kangwanda alifunga bao lililoipa Yanga ushindi dhidi ya watani wao wa jadi, katika mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.
Mchezo huo uliwakutanisha Yanga, mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26, na Simba, mabingwa wa Kombe la shirikisho, katika kuwania taji la kwanza la msimu wa 2026/27.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuanza msimu mpya kwa kutwaa Ngao ya Jamii, huku ikiendeleza rekodi yake nzuri dhidi ya Simba katika mashindano hayo.
Katika Ngao ya Jamii ya mwaka 2025, Yanga pia iliifunga Simba kwa bao 1-0.

0 Comments