DUNIA ITASHUHUDIA KUPATWA KWA JUA LEO

 Dunia leo Jumatano, Agosti 12, 2026, inashuhudia tukio la nadra la kupatwa kwa Jua kwa jumla, linalotokea wakati Mwezi unapita kati ya Dunia na Jua na kulifunika Jua kwa muda.

GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA YAKO CHUMBANI SASA

Kupatwa kwa Jua kwa jumla kunaonekana katika maeneo mbalimbali yaliyo kwenye njia ya kivuli cha Mwezi, yakiwemo Iceland, Greenland, kaskazini mwa Hispania na sehemu ya Ureno. Katika maeneo hayo, Mwezi utafunika kabisa uso wa Jua na kusababisha giza la muda mfupi.


Maeneo mengine ya Ulaya na Amerika Kaskazini yataweza kushuhudia kupatwa kwa Jua kwa sehemu, ambapo Mwezi utafunika sehemu tu ya Jua. Kiwango cha kupatwa kinatofautiana kulingana na eneo ambalo tukio hilo linatazamwa.

Kwa upande wa Tanzania, ikiwemo Dar es Salaam, tukio hilo halitaonekana kwa sababu nchi  haipo katika eneo la mwonekano wa kupatwa kwa Jua leo. Kilele cha kupatwa kwa Jua duniani kinatarajiwa kufikia karibu saa 17:47 UTC, sawa na saa 2:47 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Wataalamu wanawashauri watu watakaokuwa katika maeneo yanayoweza kuona kupatwa kwa Jua kutumia miwani maalum iliyotengenezwa kwa ajili ya kutazama kupatwa kwa Jua. Kutazama Jua moja kwa moja bila kinga sahihi kunaweza kusababisha madhara makubwa kwenye macho.

Post a Comment

0 Comments