RAIS SAMIA AZINDUA MWENDOKASI MBAGALA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amefungua rasmi miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya Pili inayohusisha barabara za Kilwa, Chang’ombe, Sokoine naKawawa Jijini Dar es salaam.

Katika hafla hiyo, Rais Samia ameambatana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah, hatua inayoonyesha ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na AfDB katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya miundombinu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia amesema mradi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha mfumo wa usafiri wa umma ili kukidhi mahitaji ya Wananchi na ukuaji wa Jiji la Dar es salaam.

BRT Awamu ya Pili inatarajiwa kupunguza msongamano wa magari, kufupisha muda wa safari, kuongeza ufanisi wa usafiri wa umma, pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wakazi wa Dar es salaam.



 

 

Post a Comment

0 Comments