ALI KAMWE:YANGA KUFUNGIWA KUSAJIRI SIO HABARI MPYA

 Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema hakuna sababu ya Mashabiki kuwa na hofu kuhusu taarifa zinazosambaa zikidai kuwa Klabu hiyo imefungiwa na FIFA.

Akizungumza kuelekea Maadhimisho ya Yanga Day, Kamwe amesema Viongozi wa Yanga wamechoshwa na mada hiyo kwa kuwa taratibu zote za usajili zinafanyika kupitia mfumo rasmi unaosimamiwa na mamlaka husika.

“Kuna vitu hata sisi tumechoka kuvielezea, hizi transfer zote zinafanyika katika mfumo wa portal na TFF wanafuatilia na wanajua, hivyo waulize TFF kwamba Yanga wamezuiwa,” amesema Kamwe.

Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na mijadala kuhusu taarifa za kufungiwa kwa Yanga na FIFA, huku Klabu ikiendelea na maandalizi ya Yanga Day, tukio la kila mwaka linalowakutanisha Mashabiki kwa ajili ya utambulisho wa kikosi, burudani mbalimbali na maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.


 

Post a Comment

0 Comments