MTOTO AGOMEA MKANDA,SAFARI YA NDEGE YASITISHWA

Safari ya ndege ya kampuni ya Porter Airlines nchini Canada imelazimika kusitisha safari baada ya mtoto mdogo kukataa kufunga mkanda wa usalama kabla ya kuondoka, hali iliyozua mjadala kuhusu taratibu za usalama kwa watoto wanaosafiri kwa ndege.


Tukio hilo lilitokea Agosti 6, 2026 wakati ndege hiyo ikiwa imejiandaa kuondoka kutoka Victoria kuelekea Toronto. Kwa mujibu wa kampuni hiyo, ndege ilirejeshwa katika eneo la kupandia abiria baada ya mtoto kusimama kwenye kiti chake na kukataa kufunga mkanda.

Kutokana na hali hiyo, ndege hiyo haikuweza kuendelea na safari, na abiria walilazimika kupangiwa usafiri mwingine siku iliyofuata.

Porter Airlines imesema mzazi aliyekuwa akisafiri na mtoto huyo pamoja na wahudumu wa ndege walijaribu kutatua suala hilo lakini juhudi zao hazikufanikiwa.

“Katika hali hiyo, ndege isingeweza kuondoka kwa sababu haikuwa salama,” kampuni hiyo imeeleza katika taarifa yake.

 

Post a Comment

0 Comments