ARAJIGA PILATO WA KARIAKOO DERBY,NGAO YA JAMII ZANZIBAR

 Mwamuzi Ahmed Arajiga ameteuliwa kuwa mwamuzi wa kati katika mchezo wa Ngao ya Jamii unaotarajiwa kuwakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga, kesho katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

GUSA HAPA,KAMA UMEKOSA MTOTO NA REJESHA HESHIMA CHUMBANI SASA 

Arajiga atakuwa akisimamia mchezo huo muhimu unaotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka, huku timu hizo mbili zikitarajiwa kuingia uwanjani kwa lengo la kuwania taji hilo la ufunguzi wa msimu.

Katika jukumu hilo, Arajiga atasaidiwa na waamuzi wasaidizi wawili ambao ni Mohamed Mkono na Leonard Mkumbo.

Mchezo huo wa Simba dhidi ya Yanga unatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka kutokana na ushindani wa muda mrefu uliopo kati ya klabu hizo mbili kubwa nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments