MAGHOROFA MAWILI YA CCM YABOMOLEWA ARUSHA

 Katika hali isiyo ya kawaida, taharuki imetanda katika eneo la Kata ya Ngarenaro, jijini Arusha, baada ya maghorofa mawili yanayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kubomolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

 

Uamuzi huo wa ubomoaji unadaiwa kufanyika kwa lengo la kupisha upanuzi wa barabara katika eneo hilo, hatua ambayo imevuta hisia za wananchi waliokuwa wakishuhudia zoezi hilo.

Ubomoaji huo umeibua maswali na mijadala miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, huku wengi wakitaka kufahamu zaidi sababu za hatua hiyo na mpango wa upanuzi wa barabara unaotekelezwa katika eneo hilo.

Zoezi hilo linaendelea kufuatiliwa kwa karibu, huku taarifa zaidi zikitarajiwa kuhusu sababu za ubomoaji, thamani ya majengo hayo pamoja na mpango wa TANROADS katika upanuzi wa miundombinu hiyo.

TANGAZA NASI UPATE WATEJA PIGA SASA 0654414804 OFA NI ELFU 5 KWA SIKU. 

Post a Comment

0 Comments