CHALAMILA:UZEMBE NI WENU WENGINE WANATUKANWA

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema baadhi ya Watendaji wazembe wanasababisha Viongozi watukanwe na Wananchi.

 

Chalamila ameyasema hayo leo, Agosti 19, 2026 akiwa katika Stendi ya Kimataifa ya Mabasi ya Magufuli Jijini Dar es salaam wakati akizungumza kuhusu utekelezaji wa agizo la kuhamishia mabasi katika stendi hiyo.

Amesema baadhi ya Watumishi wanadaiwa kuchukua fedha na kutumia nafasi zao kuzorotesha mchakato wa kuhamisha mabasi kwenda Stendi ya Magufuli.

Amesema Serikali haitavumilia vitendo vinavyokwamisha utekelezaji wa maagizo yake, akisisitiza kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya watakaokaidi.

Post a Comment

0 Comments