KIFO CHA KOPLO MWITA NDANI YA MAHABUSU,POLISI YAFICHUA KILICHOTOKEA

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa taarifa kuhusu kifo cha askari namba H.1796 Koplo Mwita, aliyekuwa akishikiliwa kwa ajili ya uchunguzi katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Tanga.

GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA CHUMBANI NA VIKSI LOTION. 

Kwa mujibu wa Polisi, askari huyo alikutwa amefariki dunia ndani ya chumba cha mahabusu katika kituo hicho Agosti 27, 2026, majira ya saa moja na dakika tatu usiku. 


Kabla ya kifo chake, Koplo Mwita pamoja na afisa mmoja na askari wengine watano walikuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kijinai.

Jeshi hilo limesema uchunguzi wa kisayansi uliofanyika kwa kushirikisha ndugu wa marehemu ulibaini kuwa chanzo cha kifo ni kukosa hewa kutokana na kujinyonga. Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Polisi Tanga imewataka wananchi, baadhi ya vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kusambaza taarifa zisizothibitishwa au kutoa hitimisho lisilotokana na matokeo rasmi ya uchunguzi.

Jeshi hilo limesema uchunguzi wa tukio unaendelea kukamilishwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.

Post a Comment

0 Comments