KIFO CHA MWANAFUNZI WALIMU 6 MBARONI

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linawashikilia Walimu sita wa Shule ya Sekondari Makongoro, Wilaya ya Bunda kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Mwanafunzi wa kidato cha sita, Petro Chisumo (23).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, tukio hilo linadaiwa kutokea Agosti 19, 2026 majira ya saa 11 alfajiri, wakati Chisumo akiwa pamoja na Wanafunzi wenzake wakitekeleza adhabu baada ya kupata ufaulu wa chini katika mitihani ya kujipima.

Polisi imesema katika utekelezaji wa adhabu hiyo, Mwanafunzi huyo alichapwa viboko na Walimu hao na baadaye kuishiwa nguvu, hali iliyosababisha kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Bunda kwa matibabu.

Hata hivyo, akiwa anaendelea kupatiwa matibabu, Chisumo alifariki dunia na mwili wake kuhifadhiwa hospitalini hapo.

Jeshi la Polisi limesema sababu halisi ya kifo chake bado inachunguzwa na itatolewa baada ya Madaktari kukamilisha uchunguzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara amewataka Wananchi kuwa watulivu wakati Jeshi hilo likishirikiana na Wataalamu kutoka Taasisi za kiuchunguzi kubaini chanzo halisi cha kifo cha Mwanafunzi huyo.

Post a Comment

0 Comments