Wagonjwa
watano wenye matatizo ya mishipa ya damu ya moyo iliyoziba (coronary
artery disease) wamefanyiwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu ya
moyo bila kusimamisha moyo (off Pump CABG).
TANGAZA BIASHARA YAKO UFIKIE MAELFU YA WATEJA KWA ELFU 5 TU.PIGA SASA 0654414804.
Upasuaji huo
umefanyika katika kambi maalumu ya siku tano iliyofanywa na watalaamu wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka
Hospitali ya Jaslok iliyopo Mumbai nchini India.
Akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa kufunga kambi hiyo jijini Dar es Salaam
Daktari Bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Alex Joseph alisema wagonjwa hao wamefanyiwa
upasuaji kwa mafaniko makubwa na wagonjwa wote wanaendelea vizuri na
matibabu ambapo wakati wowote tutawaruhusu kurejea nyumbani.
Kwa
upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya
Jaslok iliyopo Mumbai nchini India Upendra Bhalerao alisema watu wenye
matatizo ya mishipa ya damu wanapswa kufika katika taasisi hiyo ili
waweze kupatiwa matibabu mapema.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya
Health and Wellness Companion LTD Dkt. Priyank Punatar alisema Taasisi
hiyo imekuwa ikiwaleta watalaamu kutoka nchini India hivyo kuokoa fedha
nyingi ambazo zingetumika kuwasafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi.
Ushirikiano
kati ya JKCI na wataalamu kutoka Hospitali ya Jaslok unatajwa kuwa
sehemu ya juhudi za kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa za moyo
na mishipa ya damu nchini pamoja na kuongeza fursa kwa wagonjwa kupata
matibabu ndani ya Tanzania..jpeg)
0 Comments