Chama cha ACT
Wazalendo kimemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji,
kujiuzulu kufuatia kifo cha kijana Seif Mussa, anayedaiwa kuuawa baada
ya kukamatwa na askari wa Hifadhi ya Ngorongoro.
GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA CHUMBANI NA KAMA UNAHITAJI AJIRA SASA
Katika taarifa
iliyotolewa Agosti 14, 2026 na Waziri Kivuli wa Maliasili, Utalii,
Utamaduni na Michezo wa chama hicho, Emmanuel Ntobi, ACT Wazalendo
kimesema kinashutumu vikali matukio ya mauaji yanayodaiwa kufanywa na
askari wa hifadhi mbalimbali nchini, kikisema vitendo hivyo vinakiuka
haki za binadamu na utawala wa sheria.
Kwa mujibu wa taarifa
hiyo, tukio la Agosti 12, 2026 katika Hifadhi ya Ngorongoro ni sehemu ya
matukio mengi ya ukatili yanayodaiwa kufanywa na askari wa hifadhi
dhidi ya raia bila hatua za dhati za uwajibikaji.
ACT Wazalendo
imedai kuwa Seif Mussa, mwenye umri wa miaka 25, alikamatwa pamoja na
vijana wengine wawili, Salimu Haji na Abdallah Nuru, ambao walipotea
njia na kuingia katika eneo la hifadhi. Chama hicho kimesema vijana hao
walipigwa na kuteswa, huku Seif akifariki kutokana na majeraha
aliyopata.
Chama hicho kimesema kukamatwa kwa askari hao pekee
hakutoshi, kikimtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, pamoja na Kamishna
wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Abdul Razaq
Badru, kuchukua hatua za kisera na kiutendaji kutokana na matukio hayo.
0 Comments