JAMHURI YAOMBA AHIRISHO LA KESI YA LISU KISA USHAHIDI

 Shahidi wa 16 wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu, ACP Amini Mahamba amemaliza kutoa ushahidi wake leo Agosti 12, 2026 mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa Jaji Dunstan Ndunguru.

GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA YAKO CHUMBANI SASA

Shauri hilo lililopo Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam leo liliendelea kwa Lissu kumaliza maswali ya dodoso kwa shahidi kisha upande wa Jamhuri kuhoji maswali ya kusawazisha (Re-examination) kwa shahidi huyo.


Shauri hilo limeahirishwa mpaka kesho Agosti 13, 2026 saa tatu asubuhi, hatua ambayo imefikiwa baada ya upande wa Jamhuri kuomba ahirisho la kesi kwa sababu hawakujiandaa na shahidi mwingine.

Baada ya ombi hilo la upande wa Jamhuri, Lisu ameiomba mahakama kusimamia utekelezwaji wa amri ya upande wa Jamhuri kuja na mashaidi wawili kwa kuwa kesi hiyo imechelewa sana na sio kwa sababu zake binafsi bali sababu za upande wa Jamhuri hali inayosababisha yeye kuendelea kukaa gerezani bila hatia.

Post a Comment

0 Comments