Madaktari
Nchini Sri Lanka wamefanya upasuaji wa kuliondoa jiwe lenye uzito wa
kilo 3.1 kwenye kibofu cha mkojo cha Mwanaume mwenye umri wa miaka 55.
.jpeg)
Upasuaji
huo umefanyika katika Hospitali Kuu ya Trincomalee, Mashariki mwa Sri
Lanka, baada ya Mwanaume huyo kulazwa hospitalini kufuatia kupata
kiharusi ambapo Madaktari waligundua tatizo hilo baada ya kubaini kuwa
alikuwa akipata changamoto wakati wa kukojoa.
Jiwe hilo lilikuwa
na urefu wa takribani sentimita 17, likiwa na ukubwa unaokaribiana na
yai la mbuni na uzito unaokaribiana na wa Mtoto anayezaliwa, ambapo
Daktari aliyeongoza upasuaji huo, Dkt. Prahalahan Balakrishnan amesema
kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, huenda likawa miongoni mwa mawe
makubwa zaidi ya kibofu kuwahi kurekodiwa na kuondolewa kwa upasuaji.
Madaktari
wanaamini jiwe hilo lilikuwa limejikusanya kwenye kibofu cha mgonjwa
huyo kwa kipindi cha kati ya miaka mitano hadi 10, kwa sasa anaendelea
kupata matibabu hospitalini kutokana na matatizo mengine ya kiafya, huku
madaktari wakisema hali yake ni nzuri.
Hata hivyo, kwa mujibu wa
Guinness World Records, rekodi ya jiwe kubwa la kibofu lililoondolewa
ilikuwa ya jiwe lenye uzito wa kilo 1.9 na urefu wa sentimita 17.9,
lililoondolewa Nchini Brazil mwaka 2003 huku jiwe lililoondolewa Sri
Lanka likiwa na uzito mkubwa zaidi wa kilo 3.1.
0 Comments