ASANTENI SANA TAWI LA YANGA KEMONDO KWA KUNIPA KAZI NGUMU, HONGERENI SANA KWA TAMASHA ZURI LA YANGA DAY LENYE MWISHO USIOVUTIA

 📍 *FARIS BURUHANI :Ameandika,,,,,👇👇👇

Moja ya kazi ngumu niliyowahi kukutana nayo tangu nimevikwa koti hili la kuwaongoza Vijana wa Kagera ni hii sasa😂😂 

Ama hakika kazi ya UONGOZI ni kazi ngumu sanaaaa.

Baada ya Mashauriano ya siku mbili na Timu yangu ya Ufundi na kujiridhisha kwamba shughuli hii sitakiwi kuvaa jezi ya Timu hii, sasa maamuzi yakapatikana kwamba vazi la mgeni rasmi liwe  KANZU na KIBARAGASHIA🕺🫣

Ghafla baada ya kufika eneo la Tukio kumbe wananchi wameniandalia Uzi wao mpya😂 basi bana kwa maslahi mapana ya Shughuli yao nikaona isiwe tabu, wacha yaisheeee😁✋

ASANTENI YANGA TAWI LA KEMONDO🙏🙏







Post a Comment

0 Comments