WALIDHANI ALIFARIKI MIAKA 42 ILIYOPITA, GHAFLA AREJEA NA WATOTO NA WAJUKUU

 Frida Edward Moshi (58), aliyedhaniwa kuwa amefariki dunia baada ya kutoweka nyumbani kwao tangu mwaka 1984, amerejea salama na kuiletea furaha kubwa familia ya mzee Edward Herman Moshi katika Kijiji cha Wama Tarakea, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

GUSA HAPA:UPATE UTAJIRI BILA MASHARTI,MVUTO WA MAPENZI NA REJESHA MUME/MKE

Frida, ambaye ni mmoja kati ya watoto 16 wa familia hiyo, amerejea nyumbani baada ya miaka 42 ya kutojulikana alipo.

Inaelezwa kuwa Frida alitorokea jijini Nairobi nchini Kenya ambako alifanya kazi za uyaya, kabla ya kuolewa na kuhamia eneo la Kakamega, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Akiwa nchini Kenya, amefanikiwa kuanzisha familia yake ambapo hivi sasa amejaliwa kupata watoto wanne pamoja na wajukuu wawili.



Post a Comment

0 Comments