MOTO WATEKETEZA NYUMBA YA VYUMBA 17 BABATI

Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana umeteketeza nyumba ya wapangaji yenye vyumba 17 katika Mtaa wa Maisaka, Wilayani Babati mkoani Manyara, na kuacha wananchi kadhaa bila makazi baada ya kushindwa kuokoa mali zao.

GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA YAKO CHUMBANI SASA 

Mashuhuda na waathirika wa tukio hilo, akiwemo Christina Patrice, Ester Alex, na John Kelvin, wameeleza kuwa moto huo ulianza usiku wa kuamkia leo baada ya kusikia mlipuko wa ghafla uliosababisha moto kusambaa kwa kasi kwenye vyumba hivyo.


Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara, Emmanuel Kibona, amethibitisha kuwa askari waliwahi eneo la tukio na kufanikiwa kudhibiti moto huo kwa asilimia 100, huku kukiwa hakuna vifo wala majeruhi walioripotiwa.

Hata hivyo, kutokana na kupoteza mali na makazi yao yote, waathirika wa janga hilo wametoa kilio na wito kwa Watanzania na wadau mbalimbali kuwasaidia misaada ya kibinadamu ili kuweza kujikimu.

Post a Comment

0 Comments