Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, ameagiza kukamatwa kwa mmiliki na mjenzi wa jengo moja lililopo Masaki, baada ya kubainika kuwa alijenga ghorofa 13 badala ya ghorofa sita zilizoidhinishwa kwenye kibali cha ujenzi.
Akizungumza leo Agosti 6, 2026, wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria na taratibu za ujenzi, RC Chalamila alisema hatua hiyo inalenga kuruhusu uchunguzi wa kitaalamu kubaini iwapo msingi wa jengo hilo uliundwa kuhimili idadi hiyo ya ghorofa.
Amesema wataalamu wanapaswa kufanya tathmini ya haraka ya usalama wa jengo hilo, huku mmiliki na mjenzi wakishikiliwa kwa hatua za kisheria kutokana na tuhuma za kukiuka masharti ya kibali cha ujenzi.
RC Chalamila alisisitiza kuwa Serikali haitamvumilia mtu yeyote anayekiuka sheria za ujenzi, akieleza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuhatarisha usalama wa wananchi kwa kujenga kinyume na vibali walivyopewa.








0 Comments