TANZANIA imeendelea kuwa na bei nafuu ya mafuta ikilinganishwa na
Kenya, baada ya mamlaka ya nishati ya Kenya, EPRA, kutangaza bei mpya
zitakazoanza kutumika usiku wa leo, ambapo dizeli jijini Nairobi itauzwa
KSh 217.86 sawa na takribani Sh 4,474 za Tanzania kwa lita, huku
petroli ikiendelea kuwa KSh 214.03 sawa na takribani Sh 4,394 kwa lita.
TANGAZA NASI BIASHARA YAKO UFIKIE MAELFU YA WATEJA PIGA SASA 06544148094.
Bei
hizo mpya zinakuja baada ya EPRA kupunguza dizeli kwa KSh 5 kwa lita,
lakini hata baada ya punguzo hilo, mafuta nchini Kenya yanaendelea kuwa
ghali zaidi ukilinganisha na bei za Agosti nchini Tanzania.
Kwa
mujibu wa bei kikomo ziliotangazwa na EWURA na kuanza kutumika Agosti
5, 2026, jijini Dar es Salaam petroli inauzwa Sh 3,898 kwa lita, huku
dizeli ikiwa Sh 3,978 kwa lita. EWURA huchapisha bei kikomo za mafuta
kila mwezi kwa maeneo mbalimbali nchini.
Kwa ulinganisho wa
Nairobi na Dar es Salaam, dizeli nchini Kenya ni ghali kwa takribani Sh
496 kwa kila lita, wakati petroli pia ni ghali kwa takribani Sh 496 kwa
lita.
EPRA imeeleza kuwa punguzo la dizeli limetokana na gharama
ya kuagiza bidhaa hiyo kushuka kwa asilimia 13.08, huku gharama ya
mafuta ya taa ikishuka kwa asilimia 11.01.
Kinyume chake, gharama
ya kuagiza Super Petrol ilipanda kwa asilimia 6.99, lakini bei yake
haikupandishwa kutokana na hatua za Serikali ya Kenya za kutuliza bei.
Serikali
ya Kenya imetumia takribani KSh 938 milioni kusaidia kuzuia ongezeko la
bei za petroli na mafuta ya taa. Hata hivyo, ulinganisho wa bei mpya
unaendelea kuipa Tanzania nafasi nzuri zaidi kwa unafuu wa bei za
petroli na dizeli kati ya nchi hizo mbili, jambo lenye umuhimu mkubwa
kwa gharama za usafirishaji, uzalishaji na maisha ya kila siku.
0 Comments