WYDAD WAKANUSHA TAARIFA ZA SIMBA KUHUSU SULEIMAN MWALIMU

 Na Ally Mandai

Klabu ya Wydad Athletic Club imekanusha taarifa iliyotolewa na Simba SC kuhusu kuendelea kwa mchezaji Suleiman Mwalimu kuwa sehemu ya kikosi chake. Kupitia taarifa rasmi, Wydad imesema maelezo yaliyotolewa hayalingani na hali halisi ya kimkataba ya mchezaji huyo.

GUSA HAPA,REJESHA KUJIAMINI CHUMBANI NA VIKSI LOTION   

Wydad imeeleza kuwa haijasaini mkataba wa mkopo wala makubaliano yoyote ya uhamisho wa muda na Simba kuhusu Suleiman Mwalimu. Aidha, klabu hiyo imesisitiza kuwa mchezaji huyo bado ana mkataba halali na Wydad na yupo ndani ya mipango ya kiufundi ya timu.

Klabu hiyo imeongeza kuwa itachukua hatua zote stahiki kulinda maslahi yake, huku ikiwataka mashabiki na vyombo vya habari kutegemea taarifa zinazotolewa kupitia vyanzo rasmi vya Wydad na kuepuka kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa.


 

Post a Comment

0 Comments