HECHE: HATUFANYI SIASA ZA MAIGIZO, TUNAPIGANIA UKOMBOZI WA TANZANIA

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema chama hicho kinaendelea kufanya siasa zenye lengo la kuleta mabadiliko ya kweli nchini, akisisitiza kuwa hakijihusishi na siasa za maigizo bali kinapigania ukombozi wa Tanzania.

GUSA HAPA,REJESHA KUJIAMINI CHUMBANI NA VIKSI LOTION 

Heche ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jumatano Julai 22, 2026, ambapo alisema kuwa harakati za chama hicho zinalenga kubadilisha mfumo wa nchi, licha ya changamoto zinazowakabili viongozi na wanachama wake, ikiwemo kukamatwa na kuwekwa mahabusu au gerezani.

“Kwahiyo nataka nisisitize kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA, chama chetu kama chama kikuu cha siasa cha nchi hii siasa tunazofanya ni za kwenda kubadilisha nchi hii, na zina ‘consequences’, zina madhara kwetu”, ameeleza Heche.

Aidha, Heche amewahimiza viongozi na wanachama wa CHADEMA kuendelea kuwa na msimamo na kuelewa kuwa siasa wanazozifanya zinalenga kuleta mabadiliko ya msingi nchini. Pia ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuiunga mkono CHADEMA katika juhudi zake za kusukuma ajenda ya mabadiliko.


 

Post a Comment

0 Comments