Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya
uteuzi na uhamisho wa Viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka Jumatano
Julai 22, 2026 kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu,
mabadiliko hayo yamehusisha uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu wapya ambapo
Dkt. Latifa Mohammed Khamis kutoka TANTRADE ameteuliwa kuwa Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia maswala ya Muungano.
Prisca
Burton Lwangili kutoka TAMISEMI ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Aidha,
mabadiliko hayo yamehusisha uhamisho wa Naibu Makatibu Wakuu kwenda
katika sekta na wizara nyingine za kimkakati.
Katika hatua hiyo,
Abdallah Hassan Mitawi amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais
kwenda Wizara ya Uchukuzi, huku Balozi Baraka Haran Luvanda akitolewa
Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda Wizara ya Katiba na Sheria.
Katika
uteuzi huo Dkt. Franklin Jasson Rwezimula amehamishwa kutoka Wizara ya
Katiba na Sheria kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, naye Dkt.
Maduhu Isaac Kazi akihamishwa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda
Ofisi ya Makamu wa Rais kushughulikia masuala ya Mazingira.
Katika
ngazi ya taasisi za serikali, Rais amemteua Ephraim Balozi Mafuru kuwa
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TANTRADE) akitokea Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
0 Comments