MASHIRIKA YA NDEGE ULAYA YASITISHA SAFARI ZA MASHARIKI YA KATI

 

Mashirika ya ndege ya Ulaya yameendelea kusitisha au kubadili njia za safari zake katika baadhi ya maeneo ya Mashariki ya Kati baada ya mamlaka ya usalama wa anga kuongeza tahadhari kutokana na hatari ya mashambulizi mapya kati ya Marekani na Iran.

Uamuzi huo umetolewa na Wakala wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Umoja wa Ulaya (EASA), ambao umeelekeza waendeshaji wa ndege kuepuka kutumia anga la Iran, Iraq na Lebanon hadi Agosti 31, 2026.

Katika taarifa yake ya Jumatano Julai 8, 2026, EASA imeeleza hatua hiyo imechukuliwa kutokana na hali ya usalama kutetereka tena baada ya mashambulizi kuendelea katika ukanda huo, licha ya kuwepo kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, tathmini yake imehofia uwezekano wa kuendelea kwa mashambulizi ya kijeshi endapo makubaliano yaliyopo yataanguka.

Mvutano huo umeendelea baada ya Iran na Marekani kushambuliana katika siku za karibuni, hatua iliyoongeza hofu kwa sekta ya usafiri wa anga kutokana na uwepo wa maeneo yenye hatari karibu na njia muhimu za ndege.


 

Post a Comment

0 Comments