Waziri
wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ametembela jiji la Pretoria mji wa
shughuli za serikali nchini Afrika ya Kusini katika makao makuu ya
Wizara ya Maji na Usafi wa Mazingira na kushiriki kikao kazi
kilicholenga kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu kuhusu
masuala mbalimbali yanayohusiana na utoaji wa huduma ya maji katika
jamii.
Katika kikao ujumbe wa nchi zote umejadili teknolojia
mbalimbali zinazohusiana na Sekta ya Maji na haswa teknolojia ya
kuondosha upotevu wa maji.
Kikao kimewahusisha Balozi wa
Tanzania nchini Afrika Kusini Bw. James G. Bwana, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri na wataalamu kutoka Wizara ya Maji.
0 Comments