Wakati kesho
Alhamisi ya Julai 9, 2026, Chama cha ACT- Wazalendo na Chama cha
Mapinduzi (CCM) vikitoa tamko la pamoja la maridhiano ya kisiasa
Zanzibar, chama hicho cha upinzani kimewataka wanachama wake kulipokea
kwa moyo mkunjufu tamko hilo.
Mbali na hilo, ACT Wazalendo kimewataka wanachama wake kulijadili kwa staha, na kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wake.Tamko
hilo la maridhiano litakalosainiwa Ikulu, Zanzibar linalenga kuimarisha
maridhiano, mshikamano, utulivu wa kisiasa, amani na ustawi wa kisiwa
hicho, litashuhudiwa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi na
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud.
Taarifa kwa umma
iliyotolewa leo Jumatano Julai 8,2027 na Katibu wa Habari, Uenezi na
Mawasiliano kwa Umma wa ACT Wazalendo, Salim Bimani imeeleza katika
mchakato huo, mshindi si chama fulani bali ni Zanzibar.
“Tunawashukuru
kwa dhati wananchi wa Zanzibar, hasa wanachama na wafuasi wetu wa ACT
Wazalendo, kwa kuonesha upevu mkubwa wa kisiasa, utulivu, na imani kwa
uongozi wenu katika mchakato huu uliodumu kwa miezi minane.”
“Katika hatua ya sasa, tunawaomba na kuwasihi mlipokee tamko la pamoja kwa mioyo mikunjufu,” amesema Bimani.
0 Comments