TUME HURU YA UCHAGUZI YAKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO KATA YA MZIMUNI

 Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira, tarehe 28 Mei, 2026 ametembelea na kukagua mafunzo kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura katika Kata ya Mzimuni yaliyofanyika katika ukumbi wa  Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata ya Mzimuni utakaofanyika siku ya Jumatatu tarehe 01 Juni, 2026.

 Kata hiyo na kata nyingine 11 za Tanzania Bara zitafanya uchaguzi sambamba na uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo la Ismani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa. 

Kata nyingine ni  Zongomera, Manispaa ya Kahama; Itilo, Halmashauri ya Mji wa Nzega; Ketare, Halmashauri ya Mji wa Tarime na Nyumbigwa, Halmashauri ya Mji wa Kasulu. 

Nyingine ni kata ya Kala iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi; Ziba, Halmashauri ya Wilaya Igunga; Kamsisi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele; Nyamugali, Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe; Namasakata Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Kibiti; Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na Kata ya Bwongera Halmashauri ya Wilaya ya Chato.



 

Post a Comment

0 Comments