Mwalimu Nyerere leadership school - Kibaha
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa Dar es salaam Ndugu Ally Bananga ameshiriki Kongamano la Mafunzo ya Kiuongozi kwa Vyama Sita vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(CCM -Tanzania, ZANU PF - Zimbabwe, FRELIMO - Msumbiji, MPLA - Angola, ANC - Afrika kusini na SWAPO - Namibia).
Kongamano hilo limehusisha kutoa elimu ya namna nchi zinazoendelea zinaweza kupiga hatua kubwa kiuchumi ambapo chama tawala cha China, CPC kimewasilisha Mada na kutoa uzoefu wa namna kilivyolijenga taifa hilo kuwa miongoni mwa mataifa makubwa duniani.

.jpeg)

0 Comments