Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Toba Alnason Nguvila amewasisitiza watendaji wa serikali kushughulika na utatuzi wa kero za wananchi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa umma, akibainisha kwamba kipimo cha utendaji wao wa kazi mara zote katika kumsaidia kazi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni namna wanavyohudumia na kutatua kero za wananchi katika maeneo yao ya kazi.
Dkt. Nguvila amebainisha hayo wakati akizungumza na Viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali katika Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru, akihimiza pia kufanya kazi kwa pamoja kwani katika utumishi wa umma kila mmoja ni muhimu kwa mwenzake bila kujali ukubwa wa cheo na madaraka katika kumsaidia majukumu Rais katika utatuzi wa kero za wananchi.
"Kipimo cha utendaji wako wa kazi ni kero na malalamiko ya wananchi, ukiona sehemu watu wanalalamika sana maana yake mtendaji uliyeko eneo hilo hautoshi. Ni lazima ufanye maamuzi na maamuzi hayo yazingatie sheria, kanuni na taratibu. Usiogope kufanya maamuzi kwasababu umeajiriwa eneo hilo ili ufanye maamuzi." Amesema Dkt. Nguvila.
Amesisitiza pia umuhimu wa watendaji kutosheka na mishahara yao na kuacha tamaa ambazo zimekuwa zikisababisha migogoro isiyoisha, akisisitiza nidhamu na uzingatiaji wa maadili ya kazi kwenye kila jambo pamoja na kuacha tabia za ulevi kupita kiasi kwenye jamii.
Awali Katibu Tawala huyo amefanya ziara kwenye halmashauri za mkoa wa Arusha kwa lengo la kujitambilisha na kuzungumza na watumishi wa halmashauri hizo kusikiliza kero na changamoto zao na kujadiliana kw apamoja namna bora ya kuzitatua lengo likiwa ni kujengeana uwezo na kuwa na uwelewa wa pamoja katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi.
Mkuu Wa Wilaya Longido
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Msemaji Mkuu wa Serikali
Arusha Jiji
Monduli District Council
Karatu DC

0 Comments