BAYERN MUNICH YATWAA UBINGWA WA 35 BUNDESLIGA

 Na Ally Mandai

Bayern Munich imetwaa ubingwa wa ligi kuu Ujerumani (Bundesliga) kwa mara ya 35 kufuatia ushindi mnono wa 4-2 dhidi ya VfB Stuttgart na kufikisha pointi 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwa mechi nne zilizosalia kabla ya kufungwa kwa pazia la ligi hiyo.


Borrusia Dortmund ipo nafasi ya pili alama 64 baada ya mechi 30 na ikishinda mechi zote zilizosalia itafikisha pointi 76, alama tatu nyuma ya pointi za Bayern sasa.

FT: Bayern Munich 4-2 VfB Stuttgart
⚽ 31’ Guerreiro
⚽ 33’ Jackson
⚽ 37’ Davies
⚽ 52’ Kane
⚽ 21’ Fuhrich
⚽ 89’ Andres


 

Post a Comment

0 Comments