MPANZU ASEMA "SIWEZI KUISALITI SIMBA SC KABISA"


Na Ally Mandai.

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Elie Mpanzu (Kibisawala) amefunguka sababu zilizompelekea kusaini kandarasi jipya ndani ya Simba siku litakalomweka klabuni hapo hadi mwaka 2028.

Kupitia ujumbe wenye hisia, Mpanzu amekiri kuwa mapenzi ya mashabiki wa Simba ndiyo yaliyomfanya akatae ofa nyingine na kuchagua kubaki nyumbani.

"Nikiwa na machozi machoni mwangu ninawaandikia, wapenzi mashabiki wa Simba. Ninyi ndio wafuasi bora zaidi ambao nimewahi kukutana nao. Nataka kuwashukuru kutoka moyoni mwangu kwa msaada wenu usioyumba, licha ya nyakati ngumu ambazo nimepitia. Mmekuwa mkiniamini kila wakati"

"Kutokana na ushauri wenu kwamba ninaanza kurudi kwenye mstari ndiyo maana nimeamua kutowasaliti na kuendelea na klabu. Ninawapenda nyote sana na ninawaahidi mambo mema katika siku zijazo.


 

Post a Comment

0 Comments