VIJANA WANUFAIKA FURSA ZA MIKOPO, URASIMISHAJI SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA

 Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa, Ndugu Jessica Mushama amechambua ahadi na mafanikio ya siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu aapishwe kuwa Rais.

Ndugu Jessica amezungumzia mafanikio akianza na upande wa mikopo ambayo inakwamua vijana kiuchumi, amesema tayari vikundi 1,357 vya vijana kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 imepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 16.2 

Pia Ndugu Jessica amepongeza hatua kubwa ya Serikali kutambua makundi mbalimbali ya vijana na kuyarasimisha ili kuwa katika nafasi mbalimbali za kuwezeshwa kiuchumi.

Ametaja kundi la wafanyabiashara ndogondogo  ambao katika siku 100 za Rais Dkt. Samia jumla yao 119,595 wamesajiliwa kwenye mfumo wa Wafanyabisha Ndogo Ndogo Nchini - Management Information System (WBN-MIS).

Pia Wizara ya Madini imewarasimisha wachimbaji wadogo 2,239 ambao wameanza kupata mikopo kufanya shughuli zao na Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewarasimisha wajasiriamali 4,578.

Ndugu Jessica amelitaja pia kundi la Waendesha Bodaboda na Bajaj 209,632 ndani ya siku 100 za Rais Dkt. Samia wamerasimishwa na kupatiwa leseni za kufanya kazi zao huku zoezi hilo likiendelea.

Aidha amesema mafanikio hayo ya Rais Dkt. Samia kuhakikisha maendeleo ya kila kijana yametokana na amani, upendo, umoja na mshikamano wa kila mmoja hivyo amewasihi vijana kuendelea kudumisha tunu hizo kwa maendeleo zaidi katika Serikali ya Awamu ya Sita.



Post a Comment

0 Comments