Hayo yamebainishwa wakati wa warsha ya TAKUKURU na wadau wa sekta ya Afya iliyofanyika Wilayani Bunda.
Akizungumza wakati wa warsha hiyo Dr. Andrew Masamu , Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda (Kulia) amesema kuwa kabla ya uchambuzi wa mfumo wa kielektroniki wa utoaji huduma za matibabu uliofanywa na TAKUKURU, hospitali hiyo ilikuwa inapata mapato ya *Shs. 800,000/= hadi 1,500,000/= kwa siku*
Baada ya TAKUKURU kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya mapungufu yaliyobainika mapato yamepanda na kufikia *Shs. 3,000,000/= hadi 4,000,000/= kwa siku.*
Aidha, ameipongeza TAKUKURU kwa kazi hiyo ambayo imesaidia mapato ya Hospitali kuongezeka na hivyo kuongeza tija katika utoaji huduma kwa wananchi wilayani hapo.
Vilevile amewaasa wadau wengine wanatoa huduma kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU wakati wowote kwa manufaa ya jamii wanayo ihudumia

0 Comments