https://otieu.com/4/10556571 TUZO ZA SERENGETI ZATIKISA ARUSHA

TUZO ZA SERENGETI ZATIKISA ARUSHA

Usiku wa Tuzo za Utalii na Uhifadhi “The Serengeti Awards” umefanyika Januari 31, 2026, katika Ukumbi wa Mount Meru Hotel, Arusha, ukiwakutanisha viongozi wa Serikali na wadau wa uhifadhi na utalii kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), aliyemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo Serikali ilisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kulinda mazingira na kukuza utalii endelevu.

Katika hafla hiyo, Kamishna wa Uhifadhi TFS, Prof. Dos Santos Silayo, alimkabidhi tuzo ya Mshirika Bora wa Uhifadhi (Best Conservation Partner) Mfuko wa Hifadhi ya Milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF), iliyopokelewa na Wande Kema, kama utambuzi wa mchango wao mkubwa katika uhifadhi wa bioanuai na mazingira.

Jumla ya tuzo 51 zilitolewa kwa taasisi na watu binafsi waliotoa mchango wa kipekee katika uhifadhi na utalii, sekta inayoendelea kuwa mhimili muhimu wa uchumi wa Tanzania.

 



Post a Comment

0 Comments