https://otieu.com/4/10556571 RC MANYARA AANZA KAZI BIMA YA AFYA KWA WOTE BABATI

RC MANYARA AANZA KAZI BIMA YA AFYA KWA WOTE BABATI

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, ameanza rasmi kutoa elimu ya Bima ya Afya kwa Wote (BAW) kwa wananchi wa Mji wa Babati, akitembelea nyumba kwa nyumba na mitaa mbalimbali.

RC Sendiga amekutana na vijana wa bodaboda na bajaji, wazee pamoja na kaya mbalimbali, akihamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya kama kinga dhidi ya gharama kubwa za matibabu.

Wananchi wameonyesha mwitikio chanya na kuiomba Serikali kuhakikisha huduma bora zinaendelea kupatikana katika vituo vya afya na hospitali ili bima hiyo iwe na tija kwa walengwa.

Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote umeanza rasmi Januari 26, 2026, ukilenga kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya kwa uhakika.


 

Post a Comment

0 Comments