Kufuatia
mfululizo wa majibizano ya mashambulizi kati ya mataifa ya Marekani na
Israel dhidi ya Iran na Iran nayo kujibu, ripoti mbalimbali kutoka
vyombo vya habari vya ndani vya Iran vimeripoti kifo cha kiongozi wa
taifa hilo Ali Hosseini Khamenei.
Ni zaidi ya saa 20 sasa tangu
Marekani iishambulie Iran na Iran kujibu kumekuwa na mfululizo wa
kurushiana makombora huku athari mbalimbali zikitajwa kutokea ikiwemo
kusitishwa kwa safari za anga kwenye anga la Nchi za Falme za Kirabu
kutokana na Iran kurusha makombora katika nchi za Bahrain na maeneo
mbalimbali ya UAE ikiwemo Dubai na Qatar, kwa lengo la kuvishambulia
vituo vya kivita vya Marekani pamoja na Israel.
Mapema jana
Jumamosi Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa wamefanikiwa
kumuua Ali Hosseini Khamenei lakini taarifa hiyo haikuwa imethibitishwa
wala kutangazwa na Iran.
Hata hivyo alfajiri hii ya Jumapili
ripoti zimesambaa ikiwemo video fupi kutoka Iran zikieleza kuhusu Ali
Hosseini Khamenei kuuawa mapema jana Jumamosi akiwa katika makazi yake
huku pia wanafamilia wake na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Iran
wakitajwa kufariki katika shambulio la Marekani na Israel katika makazi
ya Khamenei huko Iran.
Kwa upande mwingine usiku wa Jumapili
Machi 1, Iran inaelezwa kuushambulia mji wa Tel Aviv huko Israel
wakilenga vituo muhimu vya kijeshi.
0 Comments