MZIZE AANZA RASMI MATIBABU YA GOTI AFRIKA KUSINI

 Na Ally Mandai.

Mshambuliaji wa Yanga SC, Clement Mzize, amesafiri kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujitonesha jeraha la goti. Nyota huyo anaweza kufanyiwa upasuaji kufuatia maumivu yaliyojirudia kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Kabylie.

Kutokana na hali hiyo, Mzize hatakuwepo kwenye kikosi cha Kocha Pedro Goncalves kuelekea Kariakoo Derby dhidi ya Simba SC itakayochezwa Machi Mosi katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, jambo linaloipa Yanga pigo kubwa safu ya ushambuliaji.

TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804. 


 

 

Post a Comment

0 Comments