KOCHA WA SIMBA AANIKA MIPANGO YA KUFUNGA YANGA KABLA YA MAPUMZIKO

Na Ally Mandai.

Kocha mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameanza kutumia mkakati wa kufunga angalau mabao mawili ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza ili kuutawala mchezo mapema.

Mkakati huu umeonekana kwenye michezo ya hivi karibuni, ikiwemo ushindi wa 3-0 dhidi ya Greenland FC na 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons, huku mabao yote makuu yakifungwa kipindi cha kwanza, ikionyesha dhamira ya kumaliza kazi mapema.

Benchi la ufundi linalenga kuhakikisha timu inapata faida mapema, kuongeza kasi ya mchezo, na kupunguza presha kipindi cha pili. Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally, amesema maandalizi yamejikita katika umakini mkubwa na matumizi sahihi ya nafasi za kufunga.

Mkakati huu pia unazidisha presha kwa wapinzani, hususan kuelekea Kariakoo Derby dhidi ya Yanga SC itakayochezwa Machi Mosi katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

 

TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804. 



Post a Comment

0 Comments