LIGI KUU BARA KUENDELEA LEO SIMBA,YANGA MZIGONI

 Na Ally Mandai.

 Ligi kuu ya kabumbu Tanzania bara inaendelea kutimua vumbi leo Februari 22, 2026 kwa nne huku Mabingwa watetezi, Young Africans Sc na Simba Sc watakuwa uwanjani kwenye viwanja tofauti.

Wananchi, Young Africans Sc watakuwa wageni wa Namungo FC katika dimba la Majaliwa, Ruangwa majira ya saa 10:00 usiku wakati Mnyama Simba Sc akiwa ugenini dhidi ya Tanzania Prisons katika dimba la Jamhuri Dodoma majira ya saa 3:00 usiku.

Mapema saa 8:00 mchana kutakuwa na mtanange kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Singida Black Stars katika dimba la Jamhuri Dodoma huku Wanalambalamba, Azam FC wakiwa na kibarua ugenini dhidi ya KMC FC katika dimba la KMC Complex saa 10:15 jioni

14:00 Mtibwa Sugar 🆚 Singida Black Stars-Jamhuri, Dodoma

16:15 KMC FC 🆚 Azam FC-KMC Complex

19:00 Namungo FC 🆚 Yanga SC-Majaliwa, Ruangwa Lindi

21:00 Tanzania Prisons 🆚 Simba Sc-Jamhuri, Dodoma.

 




Post a Comment

0 Comments