USHIRIKA WA WACHAWI HAUDUMU YANATIMIA KWA HECHE KUVURUGANA NA KINA LEMA

Na. Habibu Mchange.

Kama ulikuwa hujui ni kwanini John Heche, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tanzania Bara anatumia nguvu kubwa kuonyesha kuwa chama anachokiongoza kipo salama hasa wakati huu Mwenyekiti wake Tundu Lissu yuko mahabusu basi tu tambua kuwa Heche ana haha kufunika kombe  mwanaharamu apite.


Sio siri tena manung'uniko ya Heche kuwatumia wenzake kama 'trading factors', nayeye kujidai ana akili nyingi na kujiona anastahili kupata faida kubwa kulinganisha na wenzake yanazidi kushika kasi kiasi cha kuwafanya wenyeviti wa mikoa wakutane kwa dharura kwa njia ya mtandao na kuazimia kulidhibiti suala la Makamu wao kujimilikisha kila kitu yeye na familia yake 

Ni wazi sasa Heche analalamikikiwa kukusanya pesa ndani na nje ya nchi akiwadanganya wanaompa pesa kuwa anagawana na wenzake ama kuimarisha na mapambano (akichukua kwa wanaowaunga mkono kuvuruga amani) au kuwafanya watulie (akiwadanganya baadhi ya maafisa wa serikali). 

Lakini mwisho wa siku anakula peke yake mamilioni hayo ya pesa na wenzake kuwapiga maneno

Ndio Maana hivi sasa Heche, Lema, Sugu, Boni Yai na wengine hauwezi kuwaona katika tukio moja la kupanga namna ya kumsaidia mwenyekiti wao atoke mahabusu kwani wenzake hawa wamejiridhisha wazi kuwa mwenzao anawatumia kama Daraja la kujikusanyia pesa kwa maslahi yake binafsi

Hapa ndipo unakuja msemo wa "USHIRIKA WA WACHAWI HAUDUMU" sasa hivi Lema anamuangalia Heche kama mpigaji na Heche anamuangalia Lema na wenzake kama watu wasiotosheka

Ninazo taarifa za ushahidi wa namna gani Heche amekuwa akijikusanyia mamilioni ya fedha kupitia mgongo wa wenzake lakini wenzake wanaambulia maneno na mipango mingi hasa kudanganywa

Ninafahamu namna Heche anavyohaha kutaka kuwafanya wenzake hawa aliowageuka kwa vipande vya fedha warudi nyuma akihofia mapokeo ya mwenyekiti wao wa Taifa Tundu Lissu atakapolipata faili lote la Heche kuwatumia wenzake kama Daraja la kujikusanyia maokoto huku akilazimisha masuala yote yanayohusu mijadala, kuchukua hatua za kichama, kutoa miongozo anayasimamia yeye mwenyewe na familia yake

HECHE NI MSALITI KWA ASILI

Nawakumbusha kuwa Heche kabla hajawasaliti na kuwageuka wenzake kina Lema, Sugu, Boni na wengine, tayari alishamgeuka Freeman Mbowe ambaye alitumia Muda, akili, rasilimali na jitihada kumtengeneza Heche hadi kufika alipofika

Kwa msiotambua ni kuwa Mbowe alimuingiza Heche CHADEMA na kumfanya atambulike rasmi kuanzia mwaka 2008 baada ya kufariki kwa aliyekuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tanzania Bara Chacha Zakayo Wangwe

Wangwe alifariki akiwa Mbunge wa Jimbo la Tarime na diwani wa kata ya Tarime mjini, hivyo wakati wa kufanya uchaguzi wa marudio kuziba nafazi Mbowe alimchukua Heche aliyekuwa anajiendeleza kimasomo ya ualimu chuoni SAUTI na kumfanya agombee Udiwani wa kata ya Tarime huku nafasi ya ubunge akigombea aliyekuwa mwsnyekiti wa Hakmashauri ya Tarime  Charles Mwera ambapo wote walishinda

Mbowe hakuishia hapo aliendelea kumbeba Heche mgongoni hadi kufuta matokeo ya uchaguzi wa uenyekiti wa BAVICHA ambao Heche alishindwa na David Kafulila (2009) katika uchaguzi uliofanyika Keys Hotel mbezi beach. 

Kufutwa kwa matokeo hayo kulisababisha muendelezo wa mgogoro baina ya Mbowe, Dkt. Slaa na Kafulila kiasi cha kafulila kuhama CHADEMA kuhamia NCCR MAGEUZI chama ambacho mwaka 2010 aligombelea ubunge kigoma kusini na kushinda huku Heche akishindwa kura zz maoni ubunge Tarime alipogalagazwa na Mwita Mwikwabe Waitara

Mbowe aliendelea kumbeba Heche hata pale alipojikuta akiwakata wagombea wengine wanne wa uenyekiti wa BAVICHA mwaka 2011 ambao ni Mimi Mchange, Mtela Mwampaba, Grayson Nyakarungu na Ben Saa nane ili tu Heche mtoto wake pendwa ashinde

Mtakumbuka hata Heche alivyogaragazwa na Ester Mathiko kugombea uenyekiti wa kanda ya serengeti wote wakiwa wabunge Mbowe alimteua awe mjumbe wa kamati kuu.

Hayo ni kwa uchache tu sijaeleza namna Mbowe alivyompa Heche magari ya kutembelea , kumpangia nyumba, tickets za ndege na kumfanya kama mtoto wake wa kumzaa. 

Lakini mwaka 2024 alimgeuka kama hamjui na kuhakikisha hashindi uenyekiti.

Hakuishia tu kumgeuka bali aliongoza kikosi cha matusi mitandaoni kumkejeli, kumtukana na kumfanya aonekane kama mtu asiye na maana mbele ya chama chao. Leo Mbowe haeshimiki tena hata akitoka mbele za watu anaonekana kituko na Heche aliyemtengeneza mwenyewe kwa mikono yake kugeuka shujaa 

USALITI na UNAFIKI ni kama NGOZI, haibadiliki 

Leo Heche ameendeleza UNAFIKI wake na kuwageuka wenzake alioshirikiana nao kumuangusha mbowe.

Safari hii amewageuka kwenye maokoto na uchu wa madaraka akiamini kuendelea kumuacha Lissu mahabusu makusudi kutamfanya ajijengee ushawishi mkubwa ndani ya chama.

NITARUDI TENA

MCHANGE
Mwanachama Mwandamizi wa zamani wa CHADEMA 
0762178678


Post a Comment

0 Comments