Rais mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Jakaya Kikwete, amesema Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) umeendelea kuwa chachu ya maendeleo ya elimu ya juu nchini, kwa kusaidia kuboresha miundombinu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Dkt. Kikwete amesema hayo leo Januari 8, 2026 wakati wa uzinduzi wa Jengo la taaluma na utawala katika Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyopo Buyu, Zanzibar.
Amesema jengo hilo limejengwa kwa usimamizi wa mradi huo ambao unatoa nafasi kwa wanafunzi wengi zaidi kupata elimu bora, hasa kwenye maeneo ya kimkakati kama sayansi ya bahari, ambayo ni mhimili muhimu wa uchumi wa buluu.

0 Comments