MSHAURI WA CHADEMA, DK. CHARLES KITIMA, AFUMANIWA AKIPANGA MIKAKATI NA MAKAMU MWENYEKITI WA CHADEMA, JOHN HECHE

 TAFAKURI YA ASUBUHI

Kitima ameligeuza Kanisa kuwa hakimu wa maadili mchana na mpishi wa mikakati ya chama usiku?

Imeandikwa na Chriss Kibanda ,

MSHAURI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA padri Dk. Kitima amefumwa katika pozi zito la kimkakati akiwa na makamu mwenyekiti wa chama anacholalamikiwa na waumini wake kukishauri John Heche wakiwa katika kikao kizito cha Siri wakipanga mikakati.

Taarifa za uhakika za kikao hicho na vingine vinavyoendelea kupangwa zinaeleza kuwa ni vya kupeana mirejesho ya mafanikio na changamoto  za kampeni zao za CHADEMA kutumia kanisa (kupitia Kitima), wanaharakati na wanachama wao wengine huku wakipanga namna kupata pesa nyingi zaidi za kufanikisha malengo yao ya kupindua nchi baada ya jaribio la Oktoba 29 la kuharibu uchaguzi na kupindua nchi kukwama.

Baada ya taarifa hizi kuvuja, hasira na mshangao vimetawala miongoni mwa waumini wa Kanisa wanaohoji kwa nini Padri anayeshika nafasi nyeti ndani ya TEC anaonekana kushiriki moja kwa moja katika vikao vya kimkakati vya chama cha siasa cha CHADEMA.

Waumini hao wanasema tatizo si Padri kuwa na maoni ya kisiasa, bali ni kulitumia kanisa, nafasi ya kiroho na uaminifu wa waumini kama mtaji wa siasa za chama bila idhini yao. 

Wanahoji iwapo TEC bado ni taasisi ya kiroho au imegeuzwa kuwa sehemu ya mtandao wa kisiasa kimya wa TEC na wa Padri Dk. Kitima kufuatia tuhuma hizi unaelezwa kuzidisha mashaka kuwa kuna jambo kubwa linafanyika gizani, huku waumini wakibaki kutazamwa kama watazamaji wa mchezo wasiohusishwa.

Katika mazingira haya, maswali kadhaa yanaibuka na kuhitaji majibu:

MASWALI YANAYOHITAJI MAJIBU

1. Padri Dk. Kitima anakwenda kwenye vikao vya CHADEMA kama Padri au kama mshauri wa chama?

nani aliyeipa CHADEMA ruhusa ya kulitumia kanisa kama jukwaa la kampeni na ushawishi wa kisiasa?

3. TEC inasimama wapi viongozi wake wanapoamua kushiriki vikao vya siri vya chama cha siasa?

4. wa nini mikutano hii ifanyike kwa siri kama kweli inalenga maslahi ya wananchi na waumini?

5. Waumini wasio wanachama wa CHADEMA wanapaswa kuamini vipi kanisa linalohusishwa na chama hicho?

6. Je, TEC inawakilisha waumini wote au wale wanaolingana na msimamo wa CHADEMA pekee?

7. Ni mpaka upi kati ya injili na siasa, na ni nani ameuvuka?

8. Kanisa linapochanganywa na siasa za vurugu, nani atawajibika kwa madhara yake?

9.Padri anapopanga mikakati ya chama, madhabahu yanabaki na maana gani?

10.Kwa nini TEC inakaa kimya badala ya kuweka wazi ukweli na kulinda heshima ya kanisa?

Kwa hali ilipofikia, waumini wengi wanasema hawahitaji tena hotuba za maadili, bali majibu ya moja kwa moja. 

Kanisa haliwezi kuhubiri haki hadharani huku viongozi wake wakitajwa kupanga mikakati ya kisiasa gizani. 

Dini haiwezi kuwa sauti ya dhamiri ya taifa wakati huo huo ikihusishwa na vikao vya siri vya chama kimoja cha siasa.

Waumini wanahoji:

Kama kweli hakuna jambo linalofichwa, kwa nini hakuna tamko?

Kama kanisa linasimama upande wa haki, kwa nini linaonekana kukaa upande wa chama?

Na kama Padri ni huru kushiriki siasa, kwa nini bado anabaki kubeba mamlaka ya juu ya taasisi ya dini?

Ukimya wa TEC na wa Padri Dk. Kitima hauonekani tena kama busara, bali kama dhihaka kwa waumini na uthibitisho wa mgongano wa maslahi. 

Kadri siku zinavyopita bila majibu, ndivyo taswira ya kanisa inavyozidi kuchafuka na imani ya waumini kuzidi kuyumba.

Kwa waumini wengi, huu si tena mjadala wa picha moja wala kikao kimoja ni mjadala wa mwelekeo wa kanisa zima:

Je, kanisa litabaki kuwa mahali pa sala na ukweli?

Au litakubali kugeuzwa mtandao wa kisiasa unaofanya kazi kwa siri?

ZINGATIA

Kanisa haliwezi kuwa hakimu wa maadili mchana na mpishi wa mikakati ya chama usiku.

Padri hawezi kuwa mlezi wa dhamiri za waumini na wakati huo huo mshauri wa siasa za chama.

Na TEC haiwezi kudai kusimama juu ya vyama huku ikikaa kimya inapokabiliwa na tuhuma nzito za upendeleo.

Kama ukweli upo, usemwe hadharani.

Kama kanisa halihusiki, lijitenge wazi.

Na kama mipaka imevukwa, uwajibikaji uchukue nafasi yake.

Kwa sababu historia haitasikiliza visingizio.

Waumini hawatasahau ukimya.

Na taifa haliwezi kuchezea dini kama zana ya siasa bila kulipa gharama.

Hapa ndipo mstari umechorwa.

Ni ama kanisa, au ni chama.

Haiwezi kuwa vyote kwa wakati mmoja.

Post a Comment

0 Comments