Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshughulikia Afya, Dkt. Jafar Seif, amewasili Mkoani Njombe leo Januari 7, 2026 kwa ziara maalum ya kikazi ya siku tatu mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya msingi kwa wananchi hususani zinazotolewa wa watumishi wa kada ya afya ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mpango wa huduma ya Bima ya Afya kwa Wote.
Kabla ya ziara yake mkoani humo Dkt. Seif ametembelea Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi - CCM Mkoa wa Njombe na kuteta na Watendaji wa chama na baadae amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka na wataalam wengine kwa ngazi ya Mkoa ili kupata taarifa ya mwenendo wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali katika mkoa huo.
.jpeg)

.jpeg)

0 Comments